Kama kutakuwa na ukweli kwenye kauli za rapa Azealia Banks kuhusu uhusika wa Jay-Z kwenye sakata la kupigwa risasi kwa rapa Megan Thee Stalion lililodaiwa kufanywa na Tory Lanez, pengine jambo hilo likampeleka mahakamni Jay-Z.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii rapa huyo kutoka Harlem ameweka wazi anachoamini kuwa ndio ukweli usiofahamika na wengi kuhusu kesi ya madai kuwa rapa Tory Lanez alimshambulia kwa kumpiga risasi mguuni rapa mwenzie Megan Thee Stalion.

Amesema kwamba Megan alighushi kupigwa risasi kwa madai ilikuwa ni mbinu ya uuzaji liyobuniwa na rapa Jay-Z.

Siku ya Ijumaa Mei 20 2022, Azealia Banks aliutumia ukurasa wa Twitter na kutoa maneno ambayo yalinukuliwa kama kashfa kwa Megan Thee Stallion baada ya mashabiki kugundua kwamba Megan alichapisha picha yake na Doja Cat kwenye Tuzo za Muziki za Billboard 2022 na kumtenga (crop) mwigizaji Cara Delevingne, ambaye alikuwa sehemu ya picha hiyo.

Pamoja na kuzungumza mambo kadhaa yaliyodhihirisha kuchukizwa kwake na suala hilo, Banks alimgeukia rapa Jay-Z, ambaye ni mwanzilishi wa Roc Nation, kampuni inayomsimamia Megan Thee Stalion

“Jay-Z aliutazama ujinga wako na akabadilisha Hennessy kwa chapa yake mwenyewe ya d’usee huku ukihuzunika kufiwa kwako na mama yako mzazi, hata yeye anajua hilo tu ndio unastahili.

Mbinu za uuzaji za wasanii wa kike wa Jay-Z ni mbaya sana. Zungumza unyanyasaji wa nyumbani, pata huruma ya umma, msanii kujiamini, watenge na uwatumie kama gari kwa ajenda yoyote ya wazungu, hiyo ni mbaya sana na ya kusikitisha.” amesema Azealia Banks.

CHADEMA kutoshiriki mchakato wa kutoa maoni
Soko la kisasa mazao ya uvuvi lanukia Nkasi