Hatimaye Jay Z ametangaza rasmi ujio wa albam yake mpya aliyoibatiza jina la 4:44, ikiambana na filamu iliyobatizwa jina la albam hiyo.

Filamu hiyo ya 4:44 iliyoigizwa na Mahershala Ali na Danny Glover itatoka siku moja na albam hiyo ya Hov, Juni 30 mwaka huu.

Hata hivyo, albam hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa rapa huyo aliyebahatika kupata watoto mapacha wiki hii, itaanza kuwekwa kwenye mtandao wake wa Tidal pekee.

Jay Z aliweka rekodi kwa albam yake ya mwisho wa ‘Magna Carta: Holy Grail’ aliyoiachia Julai 4, 2013. Kuifungulia njia albam yake hiyo mpya, Jigga ameachia wimbo mpya aliouita ‘Adnis’.

Video: Muft Mkuu wa Tanzania awataka wananchi kuvaa mavazi yenye heshima
Ahaha kufanya upasuaji kurudisha ‘bikira’ aokoe ndoa yake

Comments

comments