Jay Z pamoja na Meek Mill wameanzisha taasisi itakayotoa msaada wa kisheria kwa watu weusi waliofungwa jela nchini Marekani wakisadiki kuwa kuna idadi kubwa ya watu wa aina hiyo wanaotumikia vifungo kwa makosa ambayo hawakuyafanya.

Kwa mujibu wa rapa Jay Z, Tasisis hiyo hailengi kuwasidia wale ambao wamefanya makosa bali wale waliokamatwa kwa makosa ya kubambikiziwa.

Inaaminika kuwa watu weusi bado wanaendelea kukandamizwa wakibambikiwa kesi zisizowahusu. Hivyo, wasanii hao wameungana na Robert Kraft pamoja na wasanii wengine wakiunda kundi la REFORM kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

“Nataka tueleweke vyema, kama mtu amefanya makosa anapaswa kwenda jela kwa makosa yake lakini mambo haya hayana usawa na dunia nzima inajua hivyo,” amesema Jay Z.

Naye Meek Mill ambaye alikuwa jela kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kuwa katika uangalizi wa mahakama akipinga ubaguzi wa rangi, ameguswa na wazo hilo na kujiunga katika kuhakikisha linafanikiwa, akiamini kuwa litasaidia watu zaidi ya millioni moja kwa muda wa miaka mitano.

Wanamziki wengi weusi wamekuwa wakihusishwa  na matukio ya kihalifu na uuzaji madawa kulevya. Kwa mujibu wa kundi la harakati za haki za binadamu la NAACP, kwa wastani Wamarekani weusi watano zaidi hufungwa jela ikilinganishwa na idadi  ya ‘Wazungu’ wanaokutwa na msoto huo.

Joti amlilia Mama Abdul, 'mwanao sina cha kuongea'
Video: Hawa ndiyo Marais wenye ulinzi mkubwa zaidi duniani