Beyonce na Jay Z wameamua kuwapiga tafu vijana wanaofanya vizuri katika masomo yao ya elimu ya juu ambao fedha inaweza kuwa kikwazo cha kutimiza ndoto yao, kwa kuwapa $100,000 (Sawa na Sh 228,200,000) kugharamia elimu yao.

Wanandoa hao ambao wako kwenye kilele cha majina yenye mafanikio kwenye muziki wa Hip Hop na RnB duniani wametangaza wikendi iliyopita kuwa kupitia ziara yao ya ‘On the Run II’, watatoa $100,000 kwa mwanafunzi mmoja kwa kila jiji watakalopita. Hivyo, kwa ujumla watatoa $1.1 milioni.

On the Run II inatarajia kupitia majiji 11 ambayo ni Atlanta, Orlando, Miami, Arlington, New Orleans, Houston, Phoenix, Los Angeles, San Diego na Santa Clara. Fedha hizo zimelenga zaidi kulipia karo na gharama nyingine za masomo zikazolipwa chuoni.

Mwanafunzi atakayepata fedha hizo kwenye jiji husika atakuwa anachaguliwa na umoja wa klabu zilizopo vyuoni baada ya kupitishwa kwenye vipengele vya kuwa mwanafunzi anayefanya vizuri kwenye masomo yake lakini pia iwe imethibitishwa kuwa hajiwezi kifedha kugharamia masomo yake.

Fedha hizo zinatolewa kwa ushirikiano wa taasisi ya Jay Z inayoitwa ‘Shawn Carter Foundation’ na ile ya Beyonce inayoitwa ‘BeyGOOD initiative’.

Ni dhahiri kuwa uamuzi wa Jay Z na Beyonce kuwapiga tafu wanafunzi vyuoni ni majibu ya malipo ya nguvu yao inayoonekana kwenye majiji hayo ambapo ziara ya On the Run II iliathiri ratiba za baadhi ya vyuo. Baadhi ya vyuo hususan vya Carolina Kusini vilifungwa kwa muda kwa kuhofia msongamano utakaosababishwa na ziara hiyo.

Mashabiki wakiwemo wanafunzi kwa maelfu wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanakuwa sehemu ya ziara hiyo, lakini ni kama Jay na Bey wameamua kuwakumbusha pia umuhimu wa shule na kwamba wanajali maendeleo yao ya elimu.

Gary Neville amkingia kifua Mourinho
Japan kutengeneza gari ya kupaa