Magwiji na nguli wa rap waliogeuka kuwa mahasimu wakuu na kisha kurejesha hali ya amani kati yao, Nas na Jay Z wameamsha kiu ya mashabiki wao katika kipindi cha siku mbili wakihusishwa na ujio wa albam.

Jay Z ndiye wa kwanza kuuteka mtandao wa Twitter baada ya alama za namba 4:44 iliyotapaa kwenye mabango ya mitaa ya jiji la New York kuingia kwenye mjadala mitandaoni ikihusishwa na Tidal ya Jay Z, na kwamba huenda ni jina jipya la albam yake au ni muda wa kutangaza ujio mpya wa mzigo wa Hov.

Ingawa Tidal wamekaa kimya, watu wa karibu wa Jigga akiwemo Swizz Beatz walikoleza moto kwa kuweka alama hizo kwenye mitandao yao ya kijamii. Alama hiyo inaunganishwa na tetesi za awali kuwa huenda Hov akaachia ‘Blue Print 4’, kama mfululizo wa zile Blue Print.

Kwa upande wake Nas ambaye hajawahi kutoa albam tangu mwaka 2012 alipoachia ‘Life is Good’, amewaongezea kiu mashabiki katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni.

Alisema kuwa albam yake inakamilika ndani ya kipindi cha wiki mbili zijazo na kwamba inaweza kuingia sokoni katika majira ya kiangazi.

“Ndani ya wiki mbili…ndio, siku zote nasema itakuwa tayari ndani ya wiki mbili,” NAS alifunguka.

Albam za nguli hao zinasubiriwa kwa hamu na mashabiki wao, kwa kuzingatia historia yao ya muziki na kazi kubwa walizowahi kuzifanya zilizoacha alama kwenye muziki wa hip hop duniani.

Wanaoondoka African Lyon Kujulikana Juma Hili
Peter Bosz Avaa Viatu Vya Thomas Tuchel