Msanii wa muziki wa Marekani Jay-Z ameongeza jina lingine kwenye wasifu wake, ukiachana na kuwa rapa, mtunzi wa nyimbo mshindi wa Grammy, mfanyabiashara bilionea, na mtunzi wa kimataifa – sasa anafahamika kama Hall of Famer.

Jay-Z ambaye amejibatiza jina “rapper bora zaidi aliye hai” (Greatest rapper alive) Usiku wa Jumamosi Octoba 30,2021 alitambulishwa kama sehemu ya darasa la Rock & Roll Hall of Fame 2021 lililowajumuisha Foo Fighters, Carole King, Tina Turner, The Go-Gos na Todd Rundgren.

Kuingia kwa Jay Z kwenye The Rock and Roll Hall of Fame kunachagizwa na historia ya maisha ya msanii huyo kutoka alikoanzia, jitihada za kujikwamua na namna maisha yake yalivyoweza kuigusa jamii na hata kuwa mfano wa kuigwa na mamilioni ya vijana wa kizazi hiki.

Shawn Corey Carter maarufu Jayz anafahamika kwa namna alivyoweza kuyabadili maisha yake  kutoka kuwa mfanyabiashara wa madawa ya kulevya katika mitaa ya Brooklyn, New York huko nchini Marekani, mpaka kuibukia kwenye ulimwengu wa muziki wa hip hip huku akiachia nyimbo nyingi zilizokuwa na maudhui yaliyoonyesha jitihada za mapambano dhidi ya Haki za watu weusi huko Ulaya,

Miongoni mwa nyimbo zilizopata umaarufu mkubwa kutoka kwa Jay-Z ni pamoja na “Hard Knock Life,” “99 Problems”,  “Empire State of Mind” pamoja na albamu zisizopungua 13 ambazo 9 kati ya hizo zilizowahi kushika namba moja kwenye chati mbali mbali kubwa za muziki Duniani.

Kufuatia utambulisho wa video uliomjumuisha Rais Barack Obama, LeBron James na David Letterman, Jay-Z alitambulishwa na mchekeshaji maarufu nchini humo Dave Chappelle, ambaye alimsifu kwa kuwa miongoni mwa wasanii wa mfano wa kuigwa na kuwa maisha yake yamekuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wengi nchini Marekani.

Unaweza kuwa unajiuliza hii Rock and Roll Hall of Fame ni nini ?

Rock and Roll Hall of Fame (RRHOF)  ambayo wakati mwingine huitwa Rock Hall, ni jumba la makumbusho la watu mashuhuri lililoko katikati mwa jiji la Cleveland, Ohio, nchini Marekani, kwenye kando ya Ziwa Erie.

Hili Jumba la makumbusho lenye kukusanya historia ya muziki wa Rock na wasanii, watayarishaji, wahandisi, na watu wengine mashuhuri ambao wana mchango kwenye eneo mbali mbali walijikita.

The Rock and Roll Hall of Fame Foundation ilianzishwa Aprili 20, mnamo mwaka 1983, na Ahmet Ertegun, mwanzilishi na mwenyekiti wa Atlantic Records.

Baada ya utafutaji wa muda mrefu wa jiji linalofaa, Cleveland ilichaguliwa mnamo mwaka 1986 kama nyumba ya kudumu ya kumbu kumbu za watu mashuhuri waliweka rekodi za kioekee kwenye kiwanda cha sanaa Hall of Fame.

Korosho kusafirishwa Bandari ya Dar es Salaam
Jakaya Kikwete ateta na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo