Mbuge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama sugu na mkewe Happyness wamepata mtoto wa kiume hivi karibuni na kumpa jina la Shwan  ikiwa na maana zawadi kutoka kwa mungu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sugu ametoa sababu ya kumuita mtoto wake Shwan  ambapo amesema kuwa ni katika harakati za kumuenzi rapa wa marekani JayZ  ambae pia ni mfanyabiashara ambae jina lake halisi ni Shwani Carter.

Aidha amesema kuwa amevutiwa na upambanaji wake hadi hapo alipofikia na kutambulika na dunia nzima huku falsafa za rapa huyo zikimsaidia Sugu kufika hapo alipo.

Tumempa mtoto wetu jina SHAWN JOSEPH MBILINYI…SHAWN (Tamka SHON) lina maana ZAWADI TOKA KWA MUNGU ( A GIFT FROM GOD)…Pia ni katika kumuenzi Msanii na mfanyabiashara maarufu duniani JAY-Z, ambaye jina lake halisi ni SHAWN CARTER… Hii ni kutokana na jinsi FALSAFA zake kuhusu HUSTLING zilivyonisaidia kufika hapa nilipo kwenye maisha. Asanteni sana,  Aliandika Sugu

Serikali haijasema mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari- Dkt. Abbas
Video: Undani tuhuma nzito za Masele, Mbuge amgomea Spika Ndugai

Comments

comments