Msanii nguli wa Maigizo hapa nchini Jacob Steven(JB) amefunguka na kusema kuwa wasanii wa bongo muvi wanaokimbilia kwenye muziki kuwa hawanana ubunifu na kusema walivamia fani hiyo ndiyo maana wameamua kuikacha.

Amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa kituo cha Dar24,habari bila mipaka mapema hii leo, JB amesema kuwa wasanii wote walioingia bila mipangilio ya kuweka malengo katika tasnia hiyo ndio wamekuwa wa kwanza kulalamika.’’Baadhi ya wasanii wa bongo movie wamekua wakikimbilia kwenye muziki wakiamini ndio sehemu itakayo walipa lakini wanashindwa kuelewa kuwa hata huko wanakokwenda bila kuweka malengo ni sawa na kazi bure’’ alisema JB.

Aidha aliongeza kuwa soko la filamu kwa sasa hapa limekua na linazidi kutanuka kila kukicha hivyo amewataka wasanii wenzie kufanya kazi kwa bidii ili wafikie  anga za kimataifa nakuitangaza Tanzania kimataifa.

Pamoja na mafanikio wanayoyapata msanii huyo alitanabaisha changamoto wanazokumbana nazo hasa katika tasnia hiyo ni kuwa na wimbi kubwa la vijana wanaojitokeza kutaka kuingia katika fani hiyo hivyo kupelekea kuwa na uhaba wa nafasi za kuwasaidia na kuzua lawama .

Video: Jambo Alilosisitiza Rais Magufuli Kwa Muda Wa Siku Tatu
Video: Mawaziri Watakiwa Kuhamia Dodoma Mara Moja