Serikali nchini Kenya imeripoti kuwa inampango wa kuondoa mifuko katika sare za polisi ikiwa na lengo la kupambana na rushwa nchini humo.

Hivyo imewataka polisi hao kushonewa sare mpya zisizo na mifuko.

Inaaminika kuwa endapo suala hilo litafuatwa na kutekelezwa, itakuwa ni vigumu sana kwa polisi wa usalama barabarani nchini Kenya kuchukua rushwa kwa raia na kuhifadhi mifukoni mwao.

Japokuwa, baadhi ya makamanda wa polisi walipata nafasi ya kuongelea suala hili na kusema kuwa sio rahisi kwa polisi kukubaliana na suala hilo kwani mifuko hiyo inawafanya kuwa na muonekano mzuri.

Hata hivyo mbali na suala hilo la kuondolewa mifuko kwa ajili ya kupambana na rushwa pia wananchi wametaka mifuko hiyo kuondolewa ili polisi waweze kufanya kazi kwa umakini mkubwa.

Watu mbalimbali wametoa maoni yao juu ya uamuzi huo kupitia mtandao wa Twitter na kusema kuwa suala la rushwa ni suala la mtu binafsi sio jambo rahisi kupambana nalo kwa kuondolewa kwa mifuko katika sare hizo, alisema George Kebut.

Huku wengine wakidai kuwa ”Sisi tunaogopa mifuko, na sio polisi,” alisema daktari mmoja.

“Hio mifuko ya makoti kama yakuekea spana,” alizungumza mtumiaji wa mtandao wa Twitter.

”Shida kuu sio urembo wa sare hizi ila ni kwa urefu wa mifuko ya haya makoti,” amesema Kuria Mtafsiri ambaye alitaka mifuko ya mashati kupunguzwa na mingine kuondolewa kabisa.

Sakata kama hilo liliikumba nchi ya Ghana mwaka 2017 ambapo rais wao Nana Ado Dankwa Aukofo alipotoa tamko la kuondolewa kwa mifuko kwenye sare za polisi nchini humo, ikiwa ni mojawapo ya mbinu ya kupambana na rushwa za polisi wa barabarani.

 

Video: Fahamu Ini linavyofanya kazi mwilini na umuhimu wake
LIVE: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akijibu Maswali ya Papo kwa Papo Bungeni Dodoma