Pilipili hoho hutumika kama kiungo kwenye mboga za aina mbalimbali majumbani, lakini je umewahi kujiuliza ni virutubisho gani hupatikana ndani ya pilipili hoho? na je kiungo hiko kina umuhimu gani kwenye mwili wa binadamu.

Fahamu faida zake katika kukinga mwili na magonjwa.

Pilipili hoho husadikika kuongeza virutubisho vya aina ya zeaxanthin na lutein, haya ni madini ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho, ugonjwa ambao hutokea pale ambao lenzi ya jicho inakuwa na uwingu.

Pia huongeza kinga ya mwili ya kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa sugu ya saratani na kupambana na magonjwa ya moyo kama vile presha ya kupanda na kushuka ambapo tafiti mbalimbali zimefanyika na kuthibitisha hili.

Je unafahamu kuwa kuna juisi ya pilipili hoho ambayo husaidia kuchuja takamwili na kutibu muwasho wa vidonda vya kooni.

Husaidia Kuimarisha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kupunguza shinikizo la damu na kuongeza kiwango cha damu mwilini.

Aidha, Pilipili hoho zina vitamini C kwa wingi hii husaidia kutibu ugonjwa wa kutokwa na damu puani na kuimarisha kinga ya mwili na kukinga dhidi ya saratani ya kibofu cha mkojo.

Pamoja na hayo yote, madaktari wa mambo ya lishe wamethibitisha kuwa pilipili hoho husaidia kupunguza mafuta yasiyo hitajika mwilini hivyo huweza kupunguzo uzito.

 

Zijue faida za parachichi katika kulinda afya yako
Mama aliyekamatwa Uhamiaji Marekani azuiwa kumzika mwanaye