Nyota wa Hollywood, Jean-Claude Van Damme ametua katika mazoezi ya Manchester City na kujumuika na wachezaji mbalimbali wa kikosi hicho.

Van Damme maarufu kama ‘Muscles from Brussels’ alijumuika na Yaya Toure, Sergio Aguero na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na kupiga picha pamoja.

Wabelgiji Vincent Kompany na Kevin De Bruyne pia walijumuika na mkali huyo hiyo jana ambaye alichangamsha sana mazoezi yao kwa kuwa wengi walionekana kufurahia kumuona.

Van Damme ametamba na filamu nyingi, baadhi ni Bloodsport, Hard Target na Universal Soldier.

Kilimanjaro Stars Yawasili Salama Addis Ababa
Soka La Brazil Lapata Bingwa Wa Mwaka 2015