Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean-Pierre Bemba, amerejea nyumbani baada ya kukaa gerezani muongo mzima jijini The Hague.

Kiongozi huyo amerejea DRC kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.

Bemba ambaye hukumu yake ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ilibatilishwa Mei mwaka huu, aliwasili katika uwanja wa ndege wa N’Djili jijini Kinshasa, ambako maelfu y wafuasi wake walikuwa wakimsubiri.

Aidha, kurejea kwa makamu huyo wa zamani wa rais na mbabe wa kivita kunatarajiwa kuutia hamasa upinzani dhidi ya rais Kabila, ambaye amekuwa madarakani tangu kuuawa kwa baba yake mwaka 2001.

Hata hivyo, kwa upande wake rais Kabila hajaweka hadharani kuwa hatowania katika uchaguzi huo mkuu ujao. kitu ambacho kinaiweka nchi hiyo katika hali ya wasiwasi.

 

Adhabu ya baba yamuua mwanaye, mahakama yamsweka jela
Gonzalo Higuain aondoka Juventus FC