Bingwa mpya wa dunia wa uzito wa welterweight, Jeff Horn amekanusha vikali kauli za wanaodai kuwa hakushinda pambano kati yake ya Manny Pacquiao, Julai 2 mwaka huu.

Horn ambaye alikuwa bondia asiyejulikana, ambaye ushindi wake umepingwa na asilimia kubwa wa watu wakiwemo watu maarufu kama bingwa wa zamani wa masumbwi uzito wa juu, Lennox Lewis na nguli wa mpira wa kikapo, Kobe Bryant, amesema ilikuwa siku yake na ameshinda kihalali.

“Siku zote kutakuwa na maneno ya hovyo ambayo watu watasema nilipata bahati au vinginevyo. Kutakuwa na maneno kuwa sikushinda pambano hilo, lakini mimi nilijisikia kama nimeshinda. Watu wengi wa Queensland wanaamini nimeshinda na dunia nzima,” alisema Horn.

Matokeo yaliyotangazwa na majaji watatu wa pambano hilo yaliyompa ushindi Horn yalionekana kutofautiana kwa kiasi kikubwa na tarakimu za kielekroniki zilizotolewa na Top Rank pamoja na matokeo yaliyotolewa na majaji wasio rasmi wa ESPN, waliompa ushindi mnono Pacquiao.

Hata hivyo, Pacquiao mwenyewe ameonesha kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na majaji wa pambano hilo, akidai kuwa anayaheshimu na akampongeza Horn.

Kambi ya Pacquiao imeendelea kushikilia msimamo kuwa bondia huyo alipokonywa ushindi wa wazi na majaji ambao iliwaita ‘wehu’.

Tayari wawili hao wamekwishakubaliana kushiriki pambano la marudiano mwaka huu ili kukata mzizi wa fitina.

Singida Utd Wanunua Basi
?Live: Majadiliano ya Kamati ya bunge kuhusu marekebisho ya sheria ya Madini