Mkazi wa kijiji cha Isesa wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Bujiku Mpeka amehukumiwa jela miaka 30 kwa kosa la kubaka, kutorosha na kuishi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16,wakati wa likizo ya corona.

Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Misungwi Esther Maliki amesema Peleka amewekwa hatiani baada ya upande wa mashtaka kupeleka mashahidi wanne akiwemo mwanafunzi mwenyewe anae soma kidato cha pili shule ya Sekondari Sumbugu.

“Tukiwa kwenye likizo ya corona Machi 22, Bujiku anipeleke kwao kijiji cha Isesa tukasalimie na tulipofika akanizuia kurudi nyumbani tukaishi nae hadi tulipokamatwa na polisi”. Amesema Mwanafunzi.

kwa upande wake mtuhumiwa aliiomba mahakama imsamehe kwani hatachukua tena mwanafunzi na kuishi nae.

Naye muendesha mashtaka Mkaguzi wa Msaidizi wa Polisi Juma Kipalo, ameiomba mahakama kuendelea kutoa adhabu kali ili ikukomesha tabia hii.

Mafuta ya mto Manonga kunufaisha wakazi wa mikoa minne
Simba SC waifuata Mtibwa Sugar kwa hasira - Picha