Mzazi Mohammed Masud (30), amehukumiwa kutumikia miaka 7 jela na Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma baada ya kupatikana na hatia ya kujemruhi mtoto wake (7) kwa moto na kumpa ulemavu.

Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo na kudai kuwa alimchoma mtoto kwa moto wa kuni baada ya majirani kumshtakia kuwa mtoto huyo alikuwa na tabia ya udokozi.

Aidha Taarifa zilizotolewa na Hospitali ya Wilaya ya Tunduru anakotibiwa majeruhi, zimebainisha kuwa hadi sasa, mtoto huyo hawezi kutembea kwa kutumia miguu yake.

Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Rehema Nyanda, amedai mahakamani kuwa mtoto huyo aligundulika kufanyiwa ukatili huo Machi 15 mwaka huu baada ya majirani kutoa taarifa za kupotea kwa mtoto.

Nyanda ameiomba Mahakama kutoa maelekezo ya mtoto huyo kupelekwa kwa mama yake mzazi mkoani Lindi ili kuepuka vitendo hivyo vya ukatili.

Burudani ya soka kurejea Juni 13
Kairuki asisitiza kilimo cha Alizeti kuokoa mamilioni ya kuagiza mafuta nje ya nchi