Jaji wa Mahakama ya Juu ya Manhattan nchini Marekani amemhukumu kifungo cha miaka saba jela mwanaume mmoja kwa kumlazimisha mpenzi wake atembee akiwa mtupu nje ya nyumba yao.

Jaji Robert Mandelbaum aliyeisoma hukumu hiyo Jumatano wiki hii dhidi ya Jasson Melo mwenye umri wa miaka 25, alisema kuwa kijana huyo alifanya kitendo cha udhalilishaji kisichovumilika.

Alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo ulionesha kuwa Melo alimpiga na kumtusi mpenzi wake huyo ambaye amezaa naye mtoto na kisha kumlazimisha atembee nje ya nyumba yao akiwa mtupu huku akimrekodi video.

Kwa mujibu wa ushahidi huo, Melo aliisambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kwamba awali alijaribu kuiuza. Imeelezwa kuwa kipande hicho cha video kinasauti ya Melo akiwa anamtukana mwanamke huyo akimuita malaya.

“Mtazamo wa Melo dhidi ya wanawake ni wa miaka ya zama za kiza,” Jaji Mandelbaum alisema kabla ya kufikia uamuzi wa kumpa kifungo Melo ambaye aliwahi kuwa mpishi katika ofisi za Umoja wa Mataifa.

Chanzo cha ugomvi na tukio hilo ni uamuzi wa mwanamke huyo kujaribu kuachana na Melo akitaka kwenda kuishi sehemu nyingine.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 5, 2018
Mohamed Salah abeba tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2017