Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Arusha, imemhukumu Isack Emily (40), kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Shilingi milioni 7 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana Rais Dkt. John Magufuli.

Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile, Wakili wa Serikali, Gaudensia Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook kwa nia ya kumtukana Magufuli.

Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia maneno yanayosema “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi bwana.”

Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa, Aagiza wasilipwe Posho wakisusa
Hizi ndizo tuhuma zinazomkabili Zitto Kabwe