Aliyewahi kuwa beki wa Young Africans, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ ameushauri Uongozi wa klabu hiyo kuhusu ujira ya kocha mpya, ambaye atarithi mikoba ya Cedrick Kaze aliyetimuliwa usiku wa kuamkia jana Jumatatu sambamba na wasaidizi wake.

Uongozi wa Young Africans ulifikia maamuzi ya kumuondoka kocha huyo kutoka nchini Burundi, baada ya kuchukizwa na matokeo ya matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ikitanguliwa na kupoteza mchezo dhidi ya Coastal Union kwa 1-0 jijini Tanga.

‘Jembe Ulaya’ amesema Uongozi wa Young Africans unapaswa kujitafakari kwa kina na kufanya maamuzi sahii ya kumuajiri kocha atakaekidhi haja ya klabu katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2020/21.

Amesema kwa upande wake anaona kuna haja ya Young Africans kuwaajiri makocha wazawa kama Mecky Maxime ambaye atasaidiana na Juma Mwambusi aliyekua msaidizi wa Kaze kabla ya kujiweka pembeni kwa sababu za kiafya.

Amesema wawili hao kama watapewa ushirikiano wa kutosha watakua na kila sababu ya kuivusha Young Africans katika kipindi hiki, ambacho bado ipo kwenye mbio zakuwania ubingwa wa Tanzania Bara, licha ya kuwa mbele kwa michezo minne dhidi ya Simba SC.

“Mwambusi amekaa na hawa wachezaji lakini pia anawafahamu vizuri, Mecky analijua soka la Bongo kwahiyo nazani ni wakati sahihi wao kupewa kwa muda timu waende nayo mpaka mwisho wa msimu, baada ya hapo ndio watajua waendelee nao au vipi”.

“Viongozi wanapaswa kuwa na maamuzi ya busara, hasa katika kipindi hiki ambacho kumekua na Pressure kubwa kutoka kwa mashabiki, kwangu mimi naamini wazawa wanatosha kabisa.” Amesema ‘Jembe Ulaya’

Mwambusi arithishwa mikoba Young Africans
Metacha azua maswali Young Africans