Wakati klabu ya Young Africans ikithibitisha kuondoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu Senzo Mazingiza, Mchambuzi wa Soka la Bongo Jemedari Said Kazumari ameibuka, na kupinga mazuri yanayotajwa kuhusu afisa huyo.

Senzo alitangazwa kuondoka Young Africans mwishoni mwa juma lililopita, kufuatia mkataba wake kufikia kikomo huku sababu za kifamilia zikitajwa kuwa sehemu ya kuondoka kwake Jangwani yalipo Makao Makuu ya klabu hiyo Kongwe Afrika Mashariki na Kati.

Jemedari amesema Senzo anaondoka Tanzania lakini hakuna lolote alilifanya katika ustawi wa soka la Bongo kwenye vilabu vya Simba SC na Young Africans, hivyo kwake haoni sababu ya Mdau huyo kutoka Afrika Kusini kuzungumzwa sana katika vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii.

Amesema Senzo amejinufaisha mwenyewe na sio vilabu hivyo, ambavyo bado vinahitaji msaada mkubwa wa kukua kwa haraka, hasa baada ya kukaa muda mrefu tangu vilipoanzishwa zaidi ya miaka 80 iliyopita
Jemedari ametoa kauli hiyo mapema leo Jumatatu (Agosti Mosi) akiwa katika Kipindi cha Sports HQ kilichorushwa hewani na Radio EFM jijini Dar es salaam.

“Senzo Mbatha hajafanya lolote Tanzania iwe kwa Simba au Yanga zaidi amejinufahisha yeye binafsi na kutengeneza CV yake ila kwa hapa Tanzania amepita kama watu wengine.”- alisema Jemedari Said

Senzo alikuja Tanzania miaka minne iliyopita akiajiriwa na Simba SC ambayo aliitumikia kwa miaka miwili na kuwa sehemu ya Viongozi walioipa mafanikio klabu hiyo msimu wa 2019/20 kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Msimu wa 2020/21 Senzo alihamia Young Africans, na kwa mara ya kwanza msimu wa 2021/22 alikuwa sehemu ya Viongozi waliopita mafanikio klabu hiyo kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Ngao ya Jamii.

Kikwete kuongoza Kamati ya Waangalizi uchaguzi Kenya
Maaskofu wasusa ibada kupinga mwaliko Viongozi mashoga