Mara nyingi watanzania hupenda kumtafsiri mtu kutokana na muonekano wake wa nje au kwa namna ambavyo wao wanamfahamu kupitia sanaa ya uigizaji au muziki, maisha ya filamu au ya muziki yana utofauti mkubwa sana na maisha halisi ya mtu nje ya sanaa, watu wengi hushindwa kutofautisha pande hizo mbili za sarafu, mfano kunatofauti kubwa kati ya Diamond Platinumz na Nassib Abdul baba wa watoto wawili.

Hivi karibuni staa wa utotoni, Hanifa Daudi maarufu kama Jenifer aliyeigiza kwenye filamu ya marehemu Steven Kanumba inayojulikana kama ”This is it” amedai kuwa siku za mwanzo alipoingia kujiunga kidato cha kwanza wanafunzi wenzake na walimu walikua wanamuogopa wakihisi kuwa ni mchawi kutokana na moja ya filamu zake aliziogiza kichawi.

”Vituko vilianza nilipoingia kidato cha kwanza nikachukuliwa na kupelekwa shule ya bweni ( boarding) iko Same sasa kulinipa shida watu walikuwa wananijalia,” amesema Jenifer

”Kuanzia walimu hadi wanafunzi walikuwa wananiona mtu wa ajabu labda ntakuwa naringa mpaka wengine wakawa hawaamini, nakusema naweza nikawa mchawi kweli wakawa wananitenga,”

Stori hiyo ina mfanano mzuri na hii ya muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya ambaye hivi karibuni  alijitangaza kuwa katika mambo anayotamani kuyafanya ni kuanzisha kanisa lake, watu walijadili mtazamo wake kwa upande hasi wakiamini kwa nafasi aliyopo hawezi kuwa mchungaji.

Lakini kwa upande wa pili wa uhalisia wa maisha ya muigizaji Irene Uwoya huenda kwa nafasi yake akawa anastahili kuwa mchungaji kama dhamira yake inavyomtuma.

Wazungu husema usihukumu kitabu kwa kuangalia jalada la nje (you can’t judge the book by its cover).

 

 

 

 

Video: Wagonjwa dawa za kulevya waongezeka
Wastaafu kuhakikiwa popote walipo Jijini Dar