Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh.Jenista Mhagama leo amezindua taasisi ya ujasilia mali na ushindani(TEEC) na kusema kuwa serikali ya awamu ya tano iko tayari kufanya kazi na taasisi hiyo.

Amesema hayo katika  uzinduzi wa taasisi hiyo mapema hii leo na kuipongeza  kwa kuanza kuzalisha ajira kwa vijana japo ilikuwa bado haijazinduliwa rasmi’’nawapongeza sana (TEEC) na nawaomba mbuni mfumo utakao wawezesha kuenea nchi nzima ili muweze kuwafikia vijana wote’’alisema Mh. Mhagama.

Aidha katika hatua nyingine Mh. Mhagama alitoa onyo kali kwa mkurugenzi anaesimamia mfuko wa fedha za  maendeleo ya vijana na watendaji wote wazembe kuwa wasifanye kazi kwa mazoea na kuagiza wafanye kazi kushirikiana na TEEC.

Kwa upande wake mwenyekiti wa taasisi hiyo bi.Beng’i Mazana Issa alisema kuwa taasisi ya ujasilia mali na ushindani inajielekeza katika kujenga utamaduni wa kujasiri mali na kuwafanya wajasilia mali si kuwa jasiri tu bali kuongeza ubunifu na kufanya bidhaa zao kuwa za ushindani.

Bi.Beng’I aliongeza kuwa taasisi imejipanga katika misingi ambayo ni kujenga na kuimarisha ushirikiano na wadau ikiwemo serikali,sekta binafsi,wana taaluma na wadau wa maendeleo.

Hata hivyo alisema kuwa mpaka sasa taasisi ya TEEC imeshatekeleza miradi miwili muhimu ambayo ni mradi wa jiajiri kijana ambao unatekelezwa na shirika la uingereza la Youth Bussines International(YBI) na wapili ni ule wa Best Dialogue wa kutafuta maoni ya wamiliki wa biashara ili kupata changamoto zinazozuia ushindani.

Kwa upande wake mkurugenzi wa  taasisi ya mamlaka ya elimu sayansi na teknolojia bw,Hassan Mshinda  alisema  sayansi na teknolojia ni kitu cha msingi sana katika ubunifu na ushindani wa kimaendeleo,hivyo kuna ulazima wa kuwekeza nguvu zote katika teknolojia.

Australia: Kijana Mwenye Miaka 18 Amudu Kuendesha Ndege Yenye Injini Moja
Donald Trump Adai Hillary Clinton Afya Yake Ni Dhaifu Hafai Kuwa Rais Wa Marekani