Klabu ya Bordeaux ya nchini Ufaransa, imekamilisha usajili wa mshambuliaji Jeremy Menez akitokea kwa wakali wa mjini Milan (AC Milan).

Menez, alishindwa kuonyesha uwezo wake akiwa na AC Milan msimu uliopita, kufuatia majeraha ya mgongo yaliyomkabili kwa muda mrefu, hali ambayo ilipelekea kucheza michezo kumi ya ligi ya nchini Italia (Sirie A).

Kusajiliwa na klabu ya Bordeaux, ni kama kunafungua safari mpya ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye atahitajika kuonyesha uwezo wake wote, kutokana na mashabiki wengi kuwa na matarajio makubwa dhidi yake.

Klabu ya Bordeaux ilimaliza katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa msimu uliopita.

” Girondins de Bordeaux, imekia makubaliano na AC Milan na kufanikiwa kumsajili mshambuliaji Jeremy Menez,” Imeandikwa katika tovuti ya klabu hiyo.

Menez, aliwahi kucheza soka nchini Ufaransa kabla ya kutimkia nchini Ufaransa mwaka 2014, ambapo aliwatumikia mabingwa wa soka nchini humo PSG kwa kipindi cha misimu mitatu.

Beenie Man aambukizwa virusi vya 'Zika', azuiwa kuingia Canada
Video: Mrema kufikisha Majina ya Polisi Wanaolazimisha Rushwa kwa Magufuli