Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amekana kumtukana Msemaji wa Simba Haji Manara na kusema kila anachosema ni kweli tupu.
Manara alifanya kikao na waandishi wa habari jana na kutishia kumfikisha Muro polisi na ikiwezekana mahakamani kutokana na kumdhalilisha huku TFF ikionekana kulifumbia macho suala hilo licha ya yeye kuwasilisha malalamiko yake.
Kwa upande wa Muro amekana tuhuma hizo kuwa alimtukana Manara na kuidhalilisha klabu ya Simba.
Muro akamtaka Manara kuchukua hatua kwani vyombo vya dola kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mahakamani ama polisi kuliko kupiga ‘porojo’.
“Kwani ni uongo kusema kocha wao amekuja kwa basi na wetu amekuja kwa ndege? Si wamemsajili kutoka Coastal pale Tanga na wetu ni Mholanzi amekuja kwa ndege,” Msemaji huyo wa Yanga alisema. “Kama anaamini amedhalilishwa aende kwenye vyombo vya dola akashtaki,” alieleza.
Chanzol: Saleh Jembe

Nadir Haroub: Nimefurahishwa Na Hatua Ya Kurudi Kwangu
Kilimanjaro Marathon Ruhusa February 28