Kamati ya maadili ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge kwa Jerry Slaa Mbunge wa jimbo la Ukonga baada ya kukutwa na makosa ya kudharau na kudhalilisha Bunge hilo.

Adhabu hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 31, Bungeni jijini Dodoma,  baada ya wabunge kuunga mkono adhabu zilizopendekezwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, dhidi ya Mbunge.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka ameliambia Bunge kuwa Slaa amefanya kosa kwa kueneza uongo kuwa Wabunge hawalipi kodi, pia kamati imeomba avuliwe uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP) kwa madai anaweza kusema uongo huko.

Taliban washerehekea kuondoka kwa Marekani
Wahandisi 17 wachukuliwa hatua