Utawala wa kijeshi nchini Guinea unatazamiwa kukumbana na shinikizo la kutangaza ratiba ya uchaguzi mpya mara baada ya kuanza kwa mikutano ya siku nne juu ya mustakbali wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wasiwasi unaongezeka kuhusu ni kwa namna gani jeshi hilo linaloongozwa na Mamady Doumbouya litaharakisha hatua ya kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia kama ilivyoagizwa na wasuluhisho wa jumuiya za kikanda na Kimataifa.

Mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea yamepongezwa kwa tahadhari na wapinzani wengine wa muda mrefu wa rais aliyeondolewa Alpha Conde,akiwemo mpinzani maarufu Cello Dalein Diallo ambaye ameshindwa mara tatu na rais Conde katika chaguzi za rais nchini humo.

Katika mkutano wa leo Jeshi lililotwaa madaraka litakutana na maafisa kutoka chama cha Diallo cha Union of Democratic Forces of Guinea na wakosoaji wengine wa Conde.

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa katika ukanda wa nchi za Afrika Magharibi na Sahel Annadif Khatir Mahammat Saleh,amesema anaweka matumaini makubwa katika mikutano hiyo ya wiki hii

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 15, 2021
Sensa ni kwa watakao lala nchini tu -Rais Samia