Jeshi la mapinduzi nchini Mali, limeahidi kuunda serikali ya mpito ya muda wa miezi 18 ili kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya mwezi uliopita dhidi ya serikali ya rais Ibrahim Boubacar Keita.

Kamati iliyoteuliwa na jeshi hilo imeidhinisha kile ilichokiita ‘mkataba wa mpito’ katika mkutano wa faragha kuhusu ubadilishanaji wa mamlaka, hatua inayotoa njia kwa serikali ya muda itakayoongoza kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi.

Hata hivyo, haijawekwa wazi kama Serikali hiyo ya mpito itaongozwa na raia au afisa wa jeshi.

Utawala wa kiraia waungwa mkono na kiongozi wa maandamano – Mali

Moussa Camara, katibu wa kamati hiyo, amesema jana kwamba serikali mpya itaundwa na wanachama zaidi ya 25, pamoja na waziri mkuu.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa chini ya mkataba wa awali, rais na mawaziri wa serikali ya mpito hawawezi kuwania madaraka muda wao wa kuhudumu utakapokamilika.

Baada ya CCM jana, ACT Wazalendo kukiwasha leo Zanzibar
Achoma nyumba ya Sh. 16 Milioni baada ya kugombana na mumewe