Jeshi la majini la Marekani limekamata silaha zilizokuwa zinaingizwa kinyume cha sheria katika Ghuba ya Aden, wakati vita vikiendelea nchini Yemen.

Mabegi yenye silaha aina ya AK-47 yamekutwa katika Boti ya kienyeji iliyokuwa inazisafirisha na zimehifadhiwa katika manowari ya kivita inayo tungua makombora iitwayo USS Jason Dunham iliyokuwa katika Ghuba ya Aden, Agosti 28, 2018.

“Meli hiyo ya kivita iliyoko pamoja na meli za Marekani za 5th Fleet, imekamata mzigo wa silaha uliokuwa unasafirishwa kinyume cha sheria ukiwa katika chombo ambacho hakimilikiwi na nchi yoyote katika eneo la bahari la kimataifa la Ghuba ya Aden,” limesema Jeshi la majini la Marekani

Aidha, tamko hilo la jeshi la Marekani limesema kuwa Manowari ya Dunham iliiona boti hiyo ambayo ni usafiri wa kienyeji majini ambao ni aghalabu kutumika katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Hata hivyo, timu ya uchunguzi na ukamataji ya meli ya Dunham ilikuta zaidi ya silaha 1,000 aina ya AK-47 zilizokuwa zimefichwa ndani ya chombo hicho.

 

Video: Matukio ya ukatili kwa Wanawake na Watoto yameongezeka- LHRC
Serikali yapanga kuzalisha Mitamba zaidi ya mil. 1 kwa mwaka