Mchekeshaji Idris Sultan anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za makosa ya kimtandao likiwemo la kujaribu kuharibu ushahidi.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema wanaendelea kumshikilia kwasababu kubwa mbili; moja ni kuwa baada ya kutakiwa kuripoti Polisi alijaribu kuharibu ushahidi na pili ni katika upelelezi wamebaini makosa mengine ya Kimtandao aliyokuwa akiyafanya.

“Katika mahojiano tuliyofanya naye tulibaini alitumia namba ya simu isiyo yake katika kutenda uhalifu huo hivyo ushirikiano wake ndio utakaomfanya aendelee kukaa kituoni” amesema Misime.

Wakili mchekeshaji huyo, Benedict Ishabakaki amesema baada ya mteja wake kuhojiwa walielezwa kuwa dhamana ipo wazi lakini kila wakifuatiliwa wanazungushwa.

Mchekeshaji huyo ambaye alikamatwa wiki iliyopita na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya kuchapisha picha ya zamani ya Rais, John Magufuli iliyoambatana na video yake akiicheka.

Mambosasa asimulia majambazi Saba walivyouawa na polisi

Dodoma FC kuanza mazoezi Al-Khamis
Burundi: Upinzani kupinga matokeo ya Urais mahakamani