JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU  YA DAR ES SALAAM LAKAMATA WATUHUMIWA SUGU

Jeshi la Polis kanda Maalumu jijini Dar es salaam limekamata watuhumiwa sugu 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi wa maungoni, wapiga debe, wavuta bangi, kikosi cha mbwa mwitu, watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na kamishina wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo, Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya operesheni kali katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Aidha pamoja na kufanikisha zoezi hilo kwa watuhumiwa hao,jeshi hilo pia wamekamata lita 952 za pombe aina ya gongo,bangi puli 227, kete 210, na misokoto144 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Katika hatua nyingine ,kikosi cha kupambana  na wizi wa simu cha polisi kimefanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa watatu(3) kwa makosa ya uporaji wa simu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kinondoni,watuhumiwa hao ni Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36),Abdallah Said (22) wote wakazi wa jijini  Dar es salaam.

Hata hivyo kamanda Sirro aligusia  zoezi zima la uhakiki wa silaha na kusema kuwa lilienda vizuri na watu walijitokeza kwa wingi japo kuna changamoto kadhaa zilizojitokeza ’’zoezi lilifanyika vizuri ingawa kulijitokeza dosari ndogo ndogo’’alisema kamanda Sirro.

Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es salaam limeweza kujikusanyia kiasi  cha shilingi 562,860,000/= kutokana na ukamataji wa makossa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia tar 15/7/2016 hadi 21/7/2016.

Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu Awataka (TCU) Na (NACTE) Kufuta Programu Kwa Vyuo Visivyosajiliwa
Trump Asema Yeye ni Sauti ya Wamarekani