Jeshi la Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara limezuia maandamano yaliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA).

Barua ya kuzuia maandamano hayo imetolewa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti, Mathew Mgema na kusema suala la kusitisha kikokotoo lilifanywa na Rais John Magufuli wakati wa hotuba yake iliyofanyika Disemba 28, 2018

Amesema kuwa badala ya kufanya maandamano hayo wameshauliwa kuwasiliana na wananchi wake wa Bunda mjini ili kupanga namna ya kumpongeza Bulaya katika eneo lake hilo la uwakilishi na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa Kwa wale wote watakaokiuka na kuonyesha dalili za uvunjifu wa amani.

Aidha, maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika Januari 9/2019 yalikuwa na nia ya kumpongeza Mbunge wa Bunda mjini kupitia tiketi ya Chadema, Ester Bulaya kwa jitihada zake za kuwatetea wastaafu katika suala la kikokotoo cha asilimia 25

Kwa upande Katibu wa (BAVICHA) Wilaya ya Serengeti, Francis Garatwa amekiri kupokea barua hiyo ya katazo la maandamano kutoka kwa Kamanda wa Polisi Wilaya hiyo.

Garatwa amesema kuwa wametii agizo kama ilivyoagizwa hivyo hawataandamana isipokuwa watafanya hivyo endapo vijana wa Chama cha Mapinduzi watapewa kibali cha kufanya maandamano kwa jambo kama hilo walilozuiwa

 

Tanesco yatoa tahadhari kwa wakazi wa Dar, Pwani na Zanzibar
JPM ampongeza IGP Sirro 'Unajitahidi'