Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 68 kati yao 62 ni wanaume na 06 ni wanawake kwa tuhuma za kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji huko katika Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Katika msako mkali uliofanywa mnamo tarehe 17.08.2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi hadi saa 18:00 jioni huko katika Kijiji cha Ngole jumla ya watuhumiwa 68 walikamatwa.

Awali mnamo tarehe 14.08.2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Ngole, Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela watuhumiwa hao kwa makusudi na bila halali waliharibu mabomba na vyanzo vya maji kwa kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya takribani Shilingi Milioni 14 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni michango ya baadhi ya wanakijiji na wafadhili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Polisi Ulrich Matei ametoa msisitizo kwa watanzania na wana Mbeya wote kuhakikisha wanalinda rasilimali ikiwemo miundombinu ya afya, elimu, barabara, maji na nishati ili kufikia malengo tarajiwa ya uchumi wa viwanda.

Milioni 600 zawaponza, sasa kupisha uchunguzi
Lugola aonya Polisi kutumiwa na mafisadi