Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshin la Polisi nchini kujiepusha na vitendo vya kuonea wananchi wanyonge wasio na hatia badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi, maadili na viapo vyao.

Nchemba amesema hayo Septemba 18, 2016 katika ziara ya siku moja Mkoani Shinyanga kukagua shughuli mbali mbali zinazofanywa na vikosi vya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

Nchemba amesema kuwaJeshi hilo linaposhindwa kuwajibika katika suala zima la isimamizi wa ulinzi na usalama wa Raia ipo hatari ya kuongezeka kwa matukio ya kijinai kwenye maeneo mengi ya nchi na kusababisha hofu kwa wananchi.

Amesema moja ya wajibu wa Jeshi la Polisi duniani kote ni kuhakikisha wananchi wanaishi katika hali ya usalama na utulivu muda wote.

Nchemba amewataka Askari Polisi hao kukumbuka agizo la Rais Magufuli la kuwatendea haki wanyonge badala ya kuwaonea au kuwadhulumu haki zao.

Vyama 12 vyataka JMP kuondoa zuio, vyatishia kutoa tamko zito
ISIS yabeba tukio la kuchomwa visu watu 9 Marekani, Mabomu yatikisa