Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam limepiga marufuku mkutano wa ndani wa viongozi wa chama cha ACT- Wazalendo uliokuwa unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PR Stadium (Karibu na Uwanja wa Taifa).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Muenezi wa Chama hicho, Ado Shaibu imesema kuwa polisi wamewalazimisha watu kutawanyika katika ukumbi huo, na kwamba hawaruhusiwi kufanya mkutano huo wa ndani.

”Leo, Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo wakiongozwa na Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe, Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif, Naibu Kiongozi wa Chama, Duni Haji walikuwa wakitarajia kukutana na wanachama wa ACT – Wazalendo katika ukumbi huu, lakini cha ajabu polisi wamejitokeza na kuwazuia,”amesema Ado Shaibu

Hata hivyo, viongozi wengine ambao wanaotarajiwa kuwa kwenye mkutano huo ni pamoja na  Mwenyekiti wa chama hicho, Yeremia Maganja, Makamu Mwenyekiti Bara, Shaaban Mambo, Katibu Mkuu, Dorothy Semu na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mtemelwa pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dar es salaam.

Polisi kigoma yakamata bunduki za kivita, risasi 125
Amshtaki bosi wake kwa kujamba ofisini

Comments

comments