Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa kikundi kinachohamasisha maandamano ambapo limesema kitendo hicho ni kinyume na sheria hivyo kwa watakao andamana watakumbana na mkono wa sheria.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani ambapo amesema kuwa kumekuwepo na kikundi ambacho kinatumia mitandao kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria na kutaka kwenda hadi Ikulu kufanya watakavyo.

“Sisi kama jeshi la polisi tunawataka kufanya mambo kwa mujibu wa sheria na siyo vinginevyo kwani kitendo cha kufanya maandamano ukiwa na nia ya kuiondoa serikali ni Uhaini. Hatua kali zitachukuliwadhidi ya watu watakaovunja sheria na tusije kulaumiwa kwa lolote,”amesema Kmishna Marijani.

Hata hivyo ameongeza kuwa anaamini wengi wanaopanga mipango hiyo ni vijana na anaamini kuwa wengi wao wameingia huko kwa kufuata mkumbo na kutaka wazazi wachukue nafasi zao kuwaonya watoto wao.

Trump aweka masharti mkutano wake na Kim
Video: Ukiivuruga Serikali unalala na njaa- Musiba