Polisi nchini Uganda imesema kuwa imewakamata watu 103 katika maandamano yaliozuka kupinga kukamatwa kwa mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la ‘Bobi Wine’ pamoja na wabunge wengine kadhaa na wanaharakati nchini humo.

Vikosi vya usalama nchini Uganda vilizima maandamano kwenye mji mkuu hapo jana Kampala kupinga kukamatwa kwa Bobi Wine.

Aidha, waandamanaji wamechoma moto magurudumu ya magari na kurusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani

Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.

Hata hivyo, watu kadhaa wamekamatwa akiwemo mwandishi wa habari wa Reuters aliyekuwa akifuatilia ghasia hizo zilizotekea jijini Kampala

 

Man Utd yalinda kibarua cha Mourinho, yaweka kando ya Zidane
Marekani, Uturuki zaendeleza ulinzi wa pamoja nchini Syria