Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amesema kuwa atalazimika kutumia Jeshi la Polisi kusimamia zoezi la usafi na ujenzi wa vyoo salama katika Kijiji cha Namasinzi, baada ya wananchi hao kushindwa kujenga vyoo hivyo.

Ameyasema hayo akiwa katika Mkutano wa hadhara alioufanya kwenye kijiji cha Namasinzi, Kata ya Kapenta, Wilayani Sumbawanga, kijiji ambacho wananchi watatu wamefariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine wakiendelea kupatiwa huduma.

Amesema kuwa ikifikia hatua hiyo Kijiji hicho kitafungiwa na hakuna atakayetoka wala kuingia na hatimaye kusitisha shughuli za kiuchumi za Kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha mpunga hali itakayopelekea maisha magumu kwa wananchi hao jambo ambalo asingependa litokee.

“Sasa tutatumia nguvu ya dola, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi katika mazingira ya usafi wala sio uchafu na kila mtu ahakikishe kwamba, mazingira anayaweka katika hali ya usafi,”amesema Wangabo

Hata hivyo, kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmshauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Dkt. Fani Musa ameishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka misaada katika bonde hilo ili kuhakikisha wanakabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu.

 

 

JPM mgeni rasmi siku ya mazingira duniani
Lewandowski atamani kuondoka Bayern Munich