Jeshi la Polisi limetaka liachwe liendelee kufanya kazi yake kwa weledi katika kushughulikia suala la Mtanzania aishiye ughaibuni, Mange Kimambi, ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwatusi mitandaoni watu mbalimbali wakiwamo viongozi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, amesema ni kweli jeshi lao linalifanyia kazi suala hilo.

“Hili jambo lina mambo mengi sana. Watu wengi wanahusika na taasisi nyingi pia zitahusika kulishughulikia, Hivyo tunaendelea kupokea mawazo ya watu mbalimbali kuhusu namna ya kwenda nalo… mawazo wanayotupa tunayafanyia kazi lakini naomba mtuache kwanza tunaendelea kulishughulikia,” amesema Mwakalukwa.

Aidha wakati Msemaji wa Polisi akisema hayo, TCRA imesema kuwa haiwezi kufunga wala kuingilia akaunti ya Kimambi kwa sababu huo siyo wajibu wake kisheria.

Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala, aliiambia Nipashe kuwa mamlaka yao haina nguvu za kisheria kufanya kazi hiyo bali wenye wajibu wa kufanya hivyo ni kitengo cha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni cha Jeshi la Polisi.

“Masuala ya akaunti za watu kwenye mitandao kama hiyo unayosema (ya Kimambi)… mwenye mamlaka ya kuingia na kuzifunga ni Jeshi la Polisi. Bunge liliipa mamlaka ya kisheria polisi kuchunguza na kukamata wahalifu kama hao… waulizeni wao,” amesema Mwakyanjala.

Hata hivyo, zipo taarifa mitandaoni zilimkariri Mtanzania huyo aishiye Marekani kuwa kilichotokea ni matokeo ya kazi ya wadukuzi wa mitandaoni, maarufu kama ‘hackers’ kupoteza akaunti yake yenye wafuasi takribani milioni 1.5.

Pamoja na hayo upo ujumbe wa lugha ya kigeni uliokuwa ukisambaa kwenye mtandao wa instagram ukionyesha kuwa akaunti inayofahamika kuwa ni ya Kimambi, imefungwa na waendeshaji wa mtandao wa Instagram kwa sababu ya kuwapo kwa malalamiko dhidi ya machapisho ya akaunti hiyo.

Video: Mbunge Nassari alivyonusurika risasi 13, Diallo akerwa Takukuru kumpekua

Comments

comments