Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kigamboni linaendealea kutoa mafunzo kwa wananchi na wafanyakazi wa makampuni na taasisi mbalimbali ili kuadhimisha vema mwaka mpya pasipo matukio na ajali za moto.

Akitoa Maelezo kwa wafanyakazi kampuni ya TIPPER, Mkaguzi  Msadizi wa Jeshi la Zimamoto Castory Willa amewaeleza namna mbalimbali za kupambana na moto kwa kutumia vifaa vya Zimamoto (Fire extinguisher).

Willa amesema kuwa wananchi wengi huwa hawapigi namba za dharula (114) kwani hawaijui jambo linalowafanya wasipate taarifa kwa wakati.

Kuhusu tatizo la Maji katika magari ya kuzimia moto, Willa  amesema huwa wanabeba maji ya kutosha lakini kinachotokea ni kwamba tenki moja la maji  huweza kuisha ndani ya dadika 3 hadi 10 kutokana na kasi ya maji yanapotoka na hivyo kuisha haraka wakati mwingine kabla moto haujazimwa kabisa.

Hata hivyo amesema mkesha wa Mwaka Mpya kutakuwa  na Gari la Zimamoto likiwa tayari ili kukabiliana na dharula yoyote itakayojitokeza kwa siku hiyo ili kuiweka Wilaya ya Kigamboni katika hali ya usalama.

Vile vile Willa, ameonya kuwa, yoyote atakae husika na kuchoma moto matairi au vitu vingine ambavyo ni hatarishi kwa usalama atachukuliwa hatua  kali za kisheria, hivyo yeyote mwenye mpango wa kufanya hivyo aache.

Afande Willa amewaomba na kuwahamasisha wananchi kuhudhuria mafunzo ya Zimamoto yatakayokuwa yakitolewa kwa nyakati tofauti na kuwa wataanza na Kata ya Kigamboni tar 31/12/2016 na Kata nyingine zitafuata. ikiwa na lengo la kujiimarisha kukabiliana na matukio ya moto

Video: Wananchi Ruangwa watakiwa kujenga vyoo, wapewa wiki mbili
Video: Lema azidi kunasa, Serikali yakata mikopo wanaosoma ng'ambo...