Jengo moja lililopo katika mtaa wa India jirani na Sabodo Parking Tower jijini Dar es salaam limeshika moto mchana huu ambapo vikosi vya zimamoto vimefika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima.

zim1

Watanzania wenye asili ya kihindi wakiwa kwenye kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

zim2

Askari wa  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

zim3

Askari wa  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakijiandaa kupokea waathirika wa janga la moto  katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi, jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

zim4

Jengo la ghorofa 12 lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi lililoshika moto na kufanikiwa kuzimwa na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,leo jijini Dar es Salaam. 

zim5

Kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kuzima moto, kuokolea watu na mali kwenye majengo marefu, kikisaidia uokoaji  katika  jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi, jijini Dar es Salaam, baada ya kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Kigoma kujengewa Mahakama Kuu
Video: Maalim Seif afunguka makubwa, aitwika zigo la lawama RITA