Jeshi la Somalia limethibitisha kutekeleza hukumu ya Mahakama ya kijeshi kwa kumuua kwa risasi hadharani mtu aliyekutwa na hatia ya kufanya ugaidi nchini humo.

Abdulkadir Abukar Shaa’ir alikutwa na hatia ya kutekeleza mauaji kwa kutumia mabomu katika sehemu mbalimbali nchini humo na alikamatwa akiwa na gari lenye vilipuzi, Desemba mwaka jana.

Voice of America imeripoti kuwa Shaa’ir ametajwa kuwa nyuma ya mashambulizi ya mabomu kwa kufanya kazi ya kusafirisha magari yenye vilipuzi kwa niaba ya Al-Shabaab. Mei 2017, alikamatwa akiwa anaendesha gari lenye vilipuzi.

Alifikishwa katika Mahakama ya kijeshi ambapo alihukumiwa kifo Desemba 6, 2017. Jeshi la Somalia limekuwa likitekeleza mara kadhaa hukumu ya adhabu ya kifo kwa kuwapiga risasi hadharani watu waliokutwa na hatia ya ugaidi.

Aliyemkimbiza bibi yake kwa fimbo atupwa jela
Wanandoa viongozi wa Serikali wafariki kwa ajali ya helikopta

Comments

comments