Klabu ya Fiorentina imestaafisha jezi namba 13 iliyokuwa ikivaliwa na nahodha wake Davide Astori kufuatia kifo cha nyota huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31.

Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Italia ( Serie A) imeweka bayana kuwa klabu ya Cagliari ambayo ni klabu ya zamani ya Astori, pia ipo kwenye mpango kama huo wa kustaafisha jezi aliyoitumia wakati wa uhai wake.

Astori alifikwa na umauti ghafla asubuhi ya Jumapili Machi 4, 2018, akiwa hotelini ambako waliweka kambi kuelekea mchezo wao wa siku hiyo wa ligi kuu soka nchini Italia dhidi ya Udinese.

Dakika moja ya ukimya itatawala kabla ya kupigwa kwa mechi za wiki hii za Klabu Bingwa Ulaya kwa ajili ya kumkumbuka mchezaji huyo ambaye pia alikuwa akiitumikia Timu ya Taifa ya Italia.

Video: Kamanda Mambosasa adai Dar es salaam iko shwari
Wallace Karia atuma salamu za pole Cyprus