Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ limeitaka timu ya Taifa ya Ubelgiji ‘De Rode Duivels’ kuondoa neno “Love” kwenye kola ya jezi zao za ugenini.

Uamuzi huo umekuja kabla ya kikosi hicho cha Roberto Martinez kucheza dhidi ya Canada, kesho Jumatano (Novemba 23) majira ya jioni, ukiwa ni mchezo wao wa kwanza katika Kombe la Dunia nchini QATAR.

FIFA hawakuwa tayari kwa mazungumzo na walikataa kabisa kujadili suala hilo na Shirikisho la Soka la Ubelgiji ‘RBFA’.

Hata hivyo ‘RBFA’ hawajaamua iwapo watakubali ombi la FIFA au laa.

Jezi hiyo imekuwa ikiuzwa kwa miezi kadhaa na imeonekana kupendwa na mashabiki, na mpango huo wa neno ‘Love’ kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinasema kuwa haukuwa na uhusiano wowote na kitambaa cha ‘OneLove’ ambacho baadhi ya timu za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ubelgiji, zilitaka kuvaa.

Ubelgiji watahitaji jezi mpya zitengenezwe na kutumwa nchini Qatar kutoka kwa kampuni ya Adidas inayotengeneza jezi hizo.

Atwoli achaguliwa tena ITUC kwa Mara ya nne Bila Kupingwa
Alious Cisse: Lawama zote nipeni mimi