Mradi wa maji yanayotokea Ruvu Chini kuanzia Octoba 10, 2021 utafika katika jimbo la Kawe baada ya ujenzi wa Matenki ya maji kujengwa jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya maji katika jimbo la Kawe

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Askofu Josephat Gwajima leo September 2, 2021 wakati akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya maji katika jimbo la kawe ikiwemo eneo la Kisanga.

Rais Samia alisimama maeneo ya Tegeta alipokuwa njiani akielekea Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani kwa kwa ajili ya kuendelea kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.

Waziri Mkenda atoa wito kwa vyama vya ushirika
Henonga atabiriwa makubwa Simba SC