Mmiliki wa klabu ya Swansea City, Jason Levien ameibuka na mawazo tofauti na viongozi wengine klabuni hapo kwa kulipendekeza jina na aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, Bob Bradley.

Levien ameibuka na jina na kocha huyo, baada ya kuafikiana na viongozi wengine kuhusu uwezo wa meneja wao wa sasa Francesco Guidolin ambao umeonyesha kutoweza kwenda sambamba na kasi ya ligi ya nchini Uingereza kama walivyotarajia.

Mmiliki huyo kutoka nchini Marekani anaamini Bradley atakua chaguo sahihi katika kipindi hiki ambapo wanahitaji kujikwamua na matokeo mabovu na kufikia azma ya kufanya vyema katika michezo inayowakabili.

Bradley, mwenye umri wa miaka 58, kwa sasa anakinoa kikosi cha Le Havre kinachoshiriki ligi daraja la pili nchini Ufaransa.

Mwishoni mwa juma lililopita taarifa zilieleza kuwa, baadhi ya viongozi wa Swansea City walimpendeleza aliyekua meneja msaidizi wa Man Utd  Ryan Giggs ambaye kwa sasa hana kazi.

Hata hivyo Bradley huenda akakabiliwa na changamoto ya kuifahamu kwa vitendo ligi ya nchini Uingereza, kwani hajawahi kufanya kazi nchini humo.

Sakata La Yaya Toure Lamgusa Baba Mzazi
Rais Magufuli awashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa