Mpango wa usajili wa beki kutoka nchini England na klabu ya Everton John Stones kujiunga na Man City ni kama umeshakamilika, kufuatia shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kupokea jina la mchezaji huyo ambalo limeorodheshwa matajiri hao wa mjini Manchester.

Stones amekua akihusishwa na mpango wa kujiunga na Man City tangu Pep Guardiola alipoanza kazi mwanzoni mwa mwezi uliopita, lakini mpaka sasa hakuna taarifa zozote za hatua za uhamisho wa beki hiyo zilizofanywa na kuthibitishwa katika vyombo vya habari.

Man City wamewasilisha orodha ya kikosi chao chenye wachezaji 21 kitakachocheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, ambapo wataanzia kwenye hatua ya mtoano kwa kucheza dhidi ya Steaua Bucuresti na jina la Stones limeonekana.

Tayari thamani ya Paunni milion 50 imeshatajwa kama ada ya uhamisho wa Stones. Kituo cha televisheni cha Sky Sports muda mcheche uliopita kimetangaza taarifa za kuonekana kwa jina la beki huyo katika orodha ya wachezaji watakaocheza michuano ya ligi ya mabingwa bara Ulaya msimu huu wakiwa na Man City.

Kisheria mchezaji anaestahili kucheza michuano hiyo ya barani Ulaya ni Yule aliyesajiliwa na klabu husika na hatoruhusiwa kucheza katika klabu nyingine yoyote ya ligi ya ndani.

Hivi karibuni Pep Guardiola aliwathibitishia waandishi wa habari kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili Stones, ambaye atajiunga na Nolito, Ilkay Gundogan, Leroy Sane, Gabriel Jesus pamoja na Oleksandr Zinchenko ambao tayari wameshatua Etihad Stadium.

Mbowe, Lissu walimwa barua na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yatakiwa kuwachukilia hatua watendaji wote waliohujumu Ushirika