Manjano ni moja ya kiungo kinachotumika  katika mchuzi lakini pia imekuwa ikitumiwa na warembo kuweka ngozi katika hali ya usafi zaidi, hutibu chunusi Manjano ina ‘antiseptic’ na ‘anti-bacterial’ ambazo husaidia kupambana dhidi ya chunusi na vidonda usoni na kukupa muonekano mzuri, manjano pia husaidia kupunguza mafuta usoni kwa wale wenye nyuso zenye mafuta.

VIfahamu vitu vinavyotakiwa kuchanganya katika manjano na hutumika kwenye urembo na hatua zake jinsi ya kutumia.

Liwa kijiko kimoja cha chai, Manjano kijiko kimoja na Juisi ya limau, changanya viungo hivi pamoja na kisha upake usoni na ukae navyo kwa muda usio pungua dakika 10, ili kuondoa chunusi, changanya manjano na maji safi kisha upake usoni na ukae hivyo kwa dakika 15 kabla ya kunawa uso wako kwa maji ya fufutende.

Lakini pia mask kwa wenye nyuso zenye mafuta mengi Manjano ina kata manufaa katika ngozi zenye mafuta na hii husaidia  kupunguza chunusi usoni.

Kama una ngozi kavu, unaweza kutengeneza ‘mask’ kwa kuchanganya ute wa yai moja, mafuta ya mizeituni vijiko viwili vya chai, namanjano vijiko viwili. Mchanganyiko huu unaweza kutumia kwenye ngozi kavu kama vile usoni, shingoni, magotini. Ukishajipaka ni muhimu uache kwa dakika 15 au 20 kabla ya kunawa.

Hata hivyo manjano ikichangaywa pamoja na viugo vingine ina ufanisi katika kuondoa makunyanzi usoni. Unaweza kuandaa mchanganyiko kwa kuchanganya unga wa manjano pamoja na mchele uliosagwa, maziwa na juisi ya nyanya na kupaka usoni na shingoni, Muda wa nusu saa ukishapita, unashauriwa kutumia maji moto kujiosha, Ukifanya hivi angalau mara moja kwa wiki uso wako utaanza kung’aa.

Pia manjano husaidia kufuta michirizi changanya manjano na maziwa au maji kisha upake katika sehemu yenye michirizi. Baada ya dakika 30, oga kwa maji ya fufutende kisha upake losheni.

Fahamu kuwa manjano husaidia katika ukuaji wa nywele, pia kuondoa mba changanya manjano na olive oil kisha upake kichwani na ukae hivyo kwa dakika 30 kabla ya kuoga, Mchanganyiko huu ukiongezwa asali pia hupunguza kukatika kwa nywele.

Hotuba ya Rais Magufuli hali ya Corona Tanzania, wagonjwa 12, wa kwanza amepona
Dkt. Tulia atembelea waliokumbwa na mafuriko Mbeya