Madakatari bingwa wa upasuaji wa moyo, mishipa ya damu na kifua kutoka taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI), wamefanya upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kutoka kifuani na kupeleka kwenye mishipa ya damu ya miguuni.

Upasuaji huo, ni kwa mara ya kwanza kufanyika nchini, ambapo mgojnwa alikuwa na tatizo la kupata maumivu makali maeneo ya miguuni, mapaja na makalio kwa muda wa miezi nane .

Baada ya uchunguzi iligundulika mshipa wa damu umeziba kabisa na kushindwa kupeleka damu kwenye miguu, damu ikawa inapelekwa kupitia mishipa midogo.

Daktari Bingwa wa upasuaji wa moyo, mishipa ya damu na kifua kutoka JKCI, Alex Joseph, amesema walimpokea mgonjwa huyo wiki iliyopita kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo visiwani Zanzibar.

Amesema, upasuaji huo umefanyika baada ya jopo la madakari bingwa kujadiliana, kushauriana na kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa mgonjwa kupona.

Video: kuna maisha baada ya uchaguzi - ACP Chatanda
Mchungaji mikononi mwa TAKUKURU