Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imesaini mkataba wa kushirikiana na jimbo la Shandong na Hospitali ya magonjwa ya Moyo ya Fuwai iliyopo jijini Beijing nchini China.

Mkataba huo ulisainiwa hivi karibuni nchini China na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi na Prof. Shengshou Hu wa jimbo la Shandong mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya wa China, Xiaowei Ma.

Aidha, makubaliano yaliyosainiwa  katika mkataba huo ni kutolewa kwa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa madaktari, wauguzi na wataalam wanaoendesha mashine za moyo (Technician) na kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo ambazo zitasaidia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa nchini.

Vilevile katika kutekeleza makubaliano hayo kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wataalam watatu ambao ni Daktari, Muuguzi na mtaalam wa kuendesha mashine za moyo (Technician) watakwenda katika Hospitali hiyo kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi.

Hata hivyo, hospitali ya Fuwai ni kituo cha kitaifa cha kutibu na chuo cha kufundisha wataalam wa magonjwa ya moyo ilianzishwa mwaka 1956  ina wodi 41, vyumba vya upasuaji wa moyo 28, vyumba vya kufanya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa njia ya kutoboa tundu dogo katika mshipa mkubwa wa paja au mkono (Cath lab) 13 na vitanda vya kulaza wagonjwa 1238.

Madiwani Watano wa Upinzani watimkia CCM
Benki ya Standard Chartered kuipatia mkopo Tanzania