Kikosi cha maafande wa JKT Ruvu, kinaendelea kujifua kwa ajili ya ligi kuu ya soka Tanzania bara ambayo kwa sasa imesimama kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Kocha wa JKT Ruvu King Abdallah Kibaden, amedhamiria kikosi chake kuendelea na mazoezi kutokana na mapungufu aliyoyaona tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi baada ya kuondoka kwa Fred Felix Minziro.

Kikosi cha maafande hao kimeweka kambi  maeneo ya Chanika kweye kituo cha michezo kinachomilikiwa na kocha Kibadeni.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa JKT Ruvu ambaye pia ni afisa mteule daraja la pili, Costantine Masanja amesema hali za wachezaji wote zipo vizuri na wana ari kubwa ya mazoezi ili kujiweka tayari kwa mchezo dhidi ya JKT Mgambo, uliopangwa kuunguruma Januari 16, kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

JKT Ruvu kwa sasa inakamata nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa kufikisha point 12 baada ya kushuka dimbani mara 13.

Facebook Wamkatalia Mbunge Kupost Picha hii
Sudan Wenyeji CECAFA Senior Challenge Cup 2016