Mkuu wa Kikosi cha JKT 833 Oljoro Luteni Kanali Joel Meidimi amewataka wahitimu wa kidato cha sita waliopangiwa kupata mafunzo ya kijeshi kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakati wa mafunzo.

Akifungua rasmi mafunzo hayo, Mkuu wa Kikosi cha JKT 833 Oljoro, Mkoani Arusha Lutein Meidimi amesema Tumewarudisha watatu nyumbani kutokana na kukutwa na ujauzito.

Aidha wahitimu wa kidato cha sita wapatao 1,366 kati ya wanafunzi 2,689 wameanza rasmi mafunzo katika kambi hiyo ya JKT Oljoro mkoani Arusha na Mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 25 septemba 2020.

Mwenyeji wa Fainali ASFC kutuma maombi TFF
14 wanaobaki Young Africans hawa hapa